Mtu mmoja amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na jiwe kubwa alipokuwa akichimba mawe katika timbo moja eneo la Athi River kaunti ya Machakos.
Mhasiriwa ambaye ni mwanaume wa makamo alikuwa akichimba mawe katika timbo la Kwakalusia eneo la Lukenya wakati ajali hiyo ilipotokea.
Chifu wa Lukenya, Tirus Musyoka, amethibisha kisa hicho.
Musyoka amesema maafisa wa polisi na wananchi walishirikiana kwa takriban saa tatu kuliondoa jiwe hilo kubwa ndipo mwili wa muhasiriwa ukaondolewa.
Musyoka aidha amewaonya wanaoendeleza kazi ya kuchimba mawe na changarawe katika timbo kujiepusha na shunghuli hizo.
Chifu huyo amesema wakati huu wa msimu wa mvua ni hatari sana kwani mchanga umekuwa mwepesi.
Mwili wa mwendazake ulichukuliwa na polisi na kupelekwa kwa kituo cha kuhifanyi maiti.
Visa vya wachimba migodi vimekuwa vikiripotiwa kwa mara nyingi hapa nchini na wengi wao hufariki baada ya kufunikwa na mchanga au hata kukosa hewa safi ya kupumua.