Mwanaume mmoja wa umri wa miaka 30 kwa kutoka kijiji cha kiong’ang’i Wilayani Nyamira Kaskazini Kaunti ya Nyamira alipatikana amefariki kitandani mwake.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Nyamira Ricah Ongare alisema kuwa mwanaume huyo alipatikani nyumbani mwake akiwa amefariki huku akisema kuwa walipoingia kwenye hiyo nyumba ya mwenda zake walipata meko uliokuwa ikiwaka na kukisia kuwa huenda meko huo ndio ulimpelekea mwanaume huyo kupoteza maisha yake kwani alikosa hewa ya kupumua.

Inasemekana kuwa mwanaume huyo alisahau meko ikiendelea kuwaka jambo ambalo lilimsababishia mwenda zake kufariki.

“Mwenda zake hakuwa na majeraha yoyote na huenda alikufa kwa kukosa hewa ya kupumua kufuatia meko ambao ni kama alilisahau kuzima kabla aanze kulala,” alihoji Afisa Ongare.

Mwili wa mwanaume huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyamira.

Afisa huyo aidha aliwaomba wakaazi wa Kaunti hiyo kuwa macho na kuzima meko iwapo wamemaliza kupika ili kuepusha kupoteza maisha yao kutokana na ukosefu wa hewa ya kupumua.

Kwa upande mwingine, wakaazi wa eneo hilo la Kiong’angi walishangazwa na kisa hicho cha kupatikana kwa mwanamme huyo amefariki na kusema ni kisa cha kusikitisha sana kwao kwani maisha ya mtu ajuaye ni Mungu.

“Tumesikitika sana kufuatia kifo cha mwanaume huyu ambaye alikuwa mtu wa heshima sana haswa kwa watu wazima na tulikuwa tunampenda sana,” alisema Mary Kenyenga mwana kijiji cha kiong’ang’i.