Mwanamme mmoja amenusurika kifo baada ya kupokea kichapo cha mbwa kutoka kwa wananchi usiku wa kuamkia Jumanne kwa kile kinadaiwa kuwa anashirikiana na wezi sugu wa ng’ombe ambao wanaendeleza wizi katika eneo la Piave mjini Njoro.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na wakaazi ni kuwa wamekerwa na wizi hususan wa ngombe ambao umekithiri katika eneo lao katika siku za hivi karibuni wakisema mshukiwa yeyote atakaye kuwa akirandaranda kwa kusudi la kufanya uharibifu watamchukulia hatua za kinidhamu.

“Tunataka hilo liwe funzo kwa yeyote mwenye nia ya kuja kutuangaisha kwa kuvuna asikopanda, hapo awali tulisema ikiwa vyombo vya usalama havitawajibika, tutachukua hatua mikononi mwetu,” alisema mkaazi mmoja ambaye alitaka jinale kubanwa.

Idaiwa kuwa mwanamme huyo alipatikana majira ya saa saba usiku na haieleweki alikokuwa akienda wala kutoka ambapo wakaazi walimpa kichapo cha mbwa kabla ya kumteketeza moto huku akiokolewa na chifu wa eneo la Piave.

Haya yamejiri huku takriban ngombe 10 wakiibwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kufuatia kile kimesemekana kuwa kudorora kwa uasalama katika eneo hilo.

Kwa sasa mshukiwa aliyetambulika kwa jina moja kama ‘Michael’ anaenedelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya jimbo la Nakuru.