Mwanaume mmoja wa umri wa makamu amefikishwa mbele ya korti mjini Eldoret kwa shtaka la kosa la mauaji.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Japheth Kerieny, almaarufu Kirinyaga, alishtakiwa kwa kosa la kumuua Felix Kimutai Novemba 22 mwezi mwaka uliopita katika soko la Pemwai, kaunti ya Baringo.

Korti iliambiwa kwamba wawili hao waligombana kwa madai yasiyojulikana, kabla ya mshtakiwa kumgonga Felix kwa chombo kiisichokua na makali kichwani na kumwacha na majeraha kabla ya mhadhiriwa kukimbizwa hospitalini alipokata kamba.

Mshtakiwa alipinga madai hayo na akaomba aachiliwe kwa dhamana, ambapo korti ilisema ipewe mda wa siku kumi na nne ili watoe uamuzi kuhusiana na swala hilo.

Uamuzi utatolewa tarehe kumi na nane mwezi Machi mwaka huu.

Kwengineko, mwanadada mmoja ameshtakiwa kwa madai ya mauaji.

Irine Kirwa alishtakiwa kumuua Emily Kirwa mnamo Januari 31 mwaka huu katika kijiji cha kapchorwa, lokesheni ya Kaplamai katika Kaunti ya Nandi.

Korti iliambiwa kwamba wawili hao walikua na mzozo wa kinyumbani kabla ya wao kupigana.

Mshtakiwa huyo alikataa madai hayo na akaomba apewe dhamana, ambapo korti iliomba mda wa majuma mawili ili kufanya uamuzi kuhusiana na dhamana hiyo.

Mashtaka hizo yaliamuliwa na Jaji George Kimondo.