Mwanasiasa Dkt Stanley Karanja kutoka Nakuru mashariki amepuuzilia mbali madai kwamba hana uhusiano mwema na Mbunge wa Nakuru mjini mashariki David Gikaria.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika kikao na wanahabari Jumatatu mjini Nakuru, Dkt Karanja, ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha ubunge Nakuru mjini mashariki anasema kuwa kando na kwamba ana mpinzani, bado hana ubaya na Gikaria. 

Anasema kuwa siasa za uhasama na uadui zilishapitwa na wakati. 

"Siasa ya sasa si ya kuwa na uhasama baina ya wawaniaji, tunafaa kufanya kazi pamoja ili kusaidia watu tunaowaakilisha," alisema Karanja. 

Wakati huo huo, amewataka wananchi kuwaheshimu viongozi walio uongozini Kwa sasa ili waweze kuhakikisha kuwa wanatimiza yale waliyoahidi.

Picha. Mwanasiasa Stanley Karanja. Amesema kuwa hana ubaya na mbunge wa Nakuru Mjini David Gikaria, kinyume na habari zilizo kwenye vyombo vya habari. PMambili/Hivisasa.com