Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani ambaye pia ni naibu kiongozi wa Chama cha Ford Kenya amesema kuwa wako tayari kugura mrengo wa Cord iwapo kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula, hatachaguliwa kupeperusha bendera ya urais wa mrengo huo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza alipozuru afisi za kampuni ya maji ya kanda ya Pwani siku ya Jumatatu ili kujulishwa kuhusu mipango ya kuunganisha maji katika eneo la Lunga Lunga, Mwashetani alisema kuwa wanaamini kama chama kuwa wana wafuasi wengi kote nchini, na hivyo basi hawafai kuonekana kama chama cha wanyonge katika mrengo huo.

Wakati huo huo, Mwashetani alitoa wito kwa viongozi katika kanda ya Pwani kushirikiana pamoja iwapo wana azma ya kutambulika kisiasa nchini.

Aidha, Mbunge huyo alisema kuwa anaunga mkono azma ya Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan joho ya kuwania kiti cha urais ifikapo mwaka wa 2022, na kusema kuwa wakati wa kanda ya Pwani kutoa rais umefika.