Mkuu wa majeshi Samson Jefwa Mwathethe ameongoza hafla ya kufuzu kwa makadeti 54 huku akiwataka kuwa waadilifu na wenye kuzingatia nidhamu ya hali ya juu.
Akizungumza katika chuo cha kijeshi cha Lanet ambapo hafla hiyo iliendelezwa, Mwathethe alikariri kuwa kufanikiwa kwa majeshi ya KDF kumepelekea Kenya kupata sifa nzuri , hatua ambayo imesaidia katika kuleta uhusiano mwema kati ya majeshi hayo na wakenya kwa jumla.
Huku akipongeza makadeti waliofuzu, Mwathethe aliwakumbusha kuwa wanafaa kuzingatia maadili mema pamoja na weledi kama njia ya kulinda sifa ya majeshi ya KDF.