Mwathiriwa wa ghashia za uchaguzi wa mwaka wa 2007-2008 ameiomba serikali kumsaidia ili kujiendeleza kimaisha.
Akiongea na Waandishi wa habari siku ya Jumatano katika hafla ya wakimbizi wanaotafuta haki ya kusaidiwa na Serikali katika uwanja wa Gusii, mwathiriwa Simeon Atandi Monyancha kutoka Bomorenda, eneo Bunge la Bonchari katika Kaunti Ya Kisii alielezea shida alizokumbana nazo katika mwaka wa 2007 wakati alikatwa mikono yake wakati wa ghashi za uchaguzi wa 2007-2008 katika sehemu ya Sotik.
Monyancha aliyekuwa na huzuni mwingi akiyasema aliyokumbana nayo wakati huo kwa sasa anaiomba Serikali kumsaidia kuweza kujipatia mapato ya kila siku.
“Naomba Serikali kunisaidia kwa kunifaidhi na pesa haswa zile zimetengwa kwa ajili ya wakimbizi ili nami niweze kujiendeleza na maisha kama wengine,” alihoji Monyancha.
Monyancha ambaye ni baba ya watoto sita na wake wawili, ilhali mkewe wa kwanza aliaga, alisema kuwa ana kibarua kigumu ya kulisha familia yake kwani hana lolote afanyalo kwa kukosa mikono zake miwili.
“Sina uwezo wa kufanya kazi kama hapo awali maanake kwa sasa sina mkono. Kazi yote hufanywa na mke wangu ambaye ambaye pia hulemewa na kazi hizo zote,” aliongezea Monyancha.
Kufuatia kuahidiwa kwa muda mrefu kuwa watafidiwa na Serikali, ahadi ambayo haijatiliwa maanani na Serikali, Monyancha sasa ameiomba Serikali kuwasaidia kwani wanaendelea kupitia machungu zaidi.
Aidha, amewaomba viongozi wanaosimamia wakimbizi kuwajali wakimbizi wote bila kuweka ubinafsi wa kujifaidi wao wenyewe.
Monyancha alisema kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuchuna majani chai alipokumbana na kisa hicho kilichomwacha bila mikono kwani alikatwa mikono na wanye walikuwa na maoni tofauti na yake kisiasa.