Mwekahazina wa chama cha Kanu Elneo Nyakiba amejitokeza kuwarahi wakazi wa kaunti ya Nyamira kuzingatia utendakazi wa gavana Nyagarama kabla ya kumchagua kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahutubia wakristo wa Parukia la kanisa Katholiki kule Nyamira siku ya Jumapili, Nyakiba alisema kuwa sharti wananchi wakague utendakazi wa gavana huyo kabla ya kumchagua kuhudumu kwenye wadhifa huo.

"Kila mara ninapokuja hapa mimi hufahamu fika kwamba gavana Nyagarama ndiye anayeshikilia wadhifa wa ugavana, na ni ombi langu kwenu kudadisi utendakazi wa Nyagarama kwenye uchaguzi mkuu ujao kabla ya kufanya maamuzi iwapo watamchagua tena," alisema Nyakiba.

Nyakiba aidha alisuta azma ya mbunge wa eneo bunge la Mugirango Magharibi James Gesami kujitoza kwenye kinyanganyiro cha kuwania ugavana akihoji kuwa sharti wananchi wachunguze utendakazi wake kwenye wadhifa wa ubunge.

"Mheshimiwa Gesami asije akafikiria kwamba anaweza tu jitoza kwenye kinyanganyiro cha kuwania ugavana bila ya wananchi kuchunguza iwapo pesa za ustawishaji maeneo bunge zimekuwa zikitumika vizuri kwa mihula miwili amekuwa akiongoza eneo bunge lake," aliongezea Nyakiba.