Kufuatia mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne wa KCSE mwaka jana kuibiwa, mwekahazina wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini John Matiang'i amejitokeza kushtumu vikali wizi huo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu kwenye shule ya upili ya Nyambaria siku ya Jumapili, Matiangi alifurahishwa na hatua ya waziri wa elimu nchini Fred Matiang'i aliyoichukua kwachisha bodi nzima ya KNEC kazi ili kuzuia mianya zaidi ya wizi. 

"Sisi chama cha Knut tumefurahishwa sana na hatua ya waziri wa elimu aliyochukua kwa kuachisha bodi nzima ya KNEC kazi na nina hakika kuwa masuala ya wizi wa mitihani yatakuwa historia humu nchini," alisema Matiang'i. 

Matiang'i aidha aliongeza kusema kuwa huenda mataifa ya kigeni yakaanza kushuku vyeti vya masomo vya humu nchini iwapo udanganyifu kwenye mitihani hautozibwa. 

"Isije ikafika kiwango kwamba mataifa ya kigeni yataanza kushuku vyeti vya masomo vya humu nchini ikiwa hali hii ya udanganyifu kwenye mitihani ya kitaifa haithadhibitiwa," aliongezea Matiang'i.