Mwekezaji katika kaunti ya Kisii ameapa kuupeleka usimamizi wa kaunti kotini kuhusiana na upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Suneka kufanywa bila mpangilio mwafaka kufwatwa na wenye mashamba yaliyoko karibu.
Abel Ongwacho amekariri kuwa kaunti ina mpango wa kufanyia upanuzi mashamba yao kwa kiwanja hicho kwa njia ya mkato, hata bila kuzingatia mstakabali waliokuwa na nao awali wa kulipia gharama ya mashamba hayo kando na kutafuta maeneo mengine mbadala.
“Naskia wanakandarasi wameambiwa kuendelea na upanuzi kwa mashambba yetu hasa shamba langu ambapo wameangusha ua ambalo lilikuwa limezunguka shamba hili bila mwelekeo ulio wazi kutolewa na kaunti,” alisema Abel.
Kulingana naye walio na mashamba yaliyoko karibu waliahidiwa kuwa watahamishwa kwa msingi wa kulipwa fidia na gharama ya hasara watakayoipitia, lakini hamna mazungumzo mengine ambayo yamefanywa na serikali kuu au ile ya kaunti.
Ameonya kuwa yeyote atakayetekeleza azimio la serikali ya kaunti kuendeleza upanuzi huo atashtakiwa kwa kukaidi swala ambalo halijafanyiwa maelewano rasmi na wahusika huku akimtaka gavana wa kaunti ya Kisii kutrilia maanani maelewano yao.