Mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo (CCU) Maur Bwanamaka akiwahutibia wanahabari hapo awali. Picha/ the-star.co.ke
Mahakama imeamrisha upande unaopinga Maur Bwanamaka kuwa mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo (CCU) kutoingilia mipango yoyote ya chama hicho hadi kesi iliyo mahakamani kwa sasa itakapoamuliwa.
Bwanamaka amesema baadhi ya watu wamekuwa wakieneza uvumi kwamba uongozi wa chama hicho umebadilishwa, hali ambayo iliwalazimu kuelekea mahakamani.Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini Mombasa, Bwanamaka alisema kwamba mahakama imewaamrisha watu hao kutojihusisha na maswala ya chama hicho mpaka kesi hiyo itakapo kamilika.Wakati huo huo, amewataka wagombea wa viti mbali mbali wanaonuia kutumia chama hicho kutokubali kulaghaiwa na watu wanaodai kuwa viongozi wa CCU.Chama hicho kimekuwa na mgogoro wa uongozi huku kesi baina ya makundi mawili yanayo ng'ang'ania uongozi ikiwa mahakamani.