Serikali imetakikiwa kutafuta suluhu la kudumu katika mzozo wa shamba la Ndabibi ADC ili kuzuia umwagaji wa damu zaidi katika shamba hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahutubia wanahabari Jumatatu mjini Nakuru, mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Nakuru Peter Ole Sono amesema kuwa ni swala la kughadhabisha kushuhudia maisha ya wanyonge yakisitishwa huku akiwataka jamii yake kushirikiana na kukaa kwa amani.

Osono amemsthumtu kiongozi nmmoja  wa enzi ya rais mustaafu Daniel Moi anayedaiwa kuileta jamii yake kutoka eneo la Kericho na kuwapa ardhi katika shamba hilo akitaja kuwa hicho ndicho chanzo cha uhasama ambao umeshuhudiwa katika siku za maajuzi na kupelekea maafa ya watu watatu katika eneo hilo

"Mbinu ya kuwadunisha na kutaka kuiondoa jamii ya Wamaasai kutoka shamba hilo wanaolitaja kama la mababu zao  tunaapa kuwa kamwe hatutakubali hatua hiyo," Sono alisema.

Mzozo wa shamba la ndabibi kati ya jamii ya Kalenjin na Maasai umeshuhudiwa katika siku za maajuzi na hata kupelekea maafa ya watu watatu huku makulima mmoja Fred Leshau aliyeuawa  akisalia katika ufuo mwezi mmoja baada ya kuuliwa na usimamizi wa shamba hilo kuchukua amri ya mahakama ya kusimamisha mazishi yake hadi pale mzozo huo utakapotatuliwa.