Vijana katika eneo bunge la Nakuru mjini mashariki wametakiwa kutumia hazina ya Uwezo kujiimarisha.
Mwenyekiti wa Uwezo katika eneo bunge la Nakuru mjini mashariki Sospeter Kariuki katika mahojiano wikendi iliyopita alisema kuwa fedha hizo zilitolewa na serikali kuwafaidi vijana.
Alisisitiza kuwa litakuwa jambo la busara iwapo vijana watatumua fursa hii kujiimarisha.
"Hizi pesa zimepeanwa na serikali kwa minajili ya vijana, na wanafaa kutumia fursa hii pasina kushrutishwa," alisema Kariuki.
Alidokeza kuwa kwa sasa wapo katika awamu ya tatu ya mpango huo na kutoa with kwa vikundi mbalimbalu kuzidi kujitolea na kutuma maombi kupata mikopo hiyo ya Uwezo.
Hata hivyo, alipongeza vikundi mbalimbali vya akina mama kwa kuonyesha nia njema ya kutaka kuimarika kutokana na mpango huo.
Aliongeza kuwa vikundi vya akina mama vimekuwa katika mstari wa mbele katika kurejesha mikopo hiyo ili kufaidi vikundi vingine.