Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa walimu wakuu wa shule za upili katika kaunti ya Kisii amesema kuwa anaunga mkono mradi wa pesa za usatwi wa maeneo bunge kwa kuwa kuna miradi mingi zinazaidia katika shule.

Akiongea siku ya Ijumaa katika uwanja wa shule ya upili ya wasichana ya Nyabururu katika hafla ya siku kuu ya elimu, Timothy Atuti alisema anaunga mkono mradi wa pesa za ustawi wa maeneo bunge kwa kuwa pesa hizo zimesaidia shule mbalimbali katika kaunti ya Kisii.

Aidha, alisema kuwa miradi mbalimbali imefanywa na pesa hizo na viwango vya masomo vimeimarika. Atuti alisisitiza kuwa pesa hizo ni muhimu kwa maendele ya shule.

Kwingineko, alisema kuwa wao kama walimu wakuu wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa uhalifu umekomeshwa shuleni.

“Tumeweka mikakati ya kuwafunza viongozi wa wanafunzi katika shule zote ili kupata mafunzo ya jinsi ya kutambua shida haswa kutoka kwa wanafunzi wenzao,”alisema Atuti.

kulingana na Atuti wanafunzi hao wakipata mafunzo hayo watakuwa na uwezo wa kutambua shida na mipango ya wanafunzi wa kutekeleza uharibifu katika shule.

Hii ni kutokana na kuwa na mikosi ya moto katika shule mbalimbali katika kaunti ya kisii ikidaiwa kuwa wanafunzi ndio wanatekeleza uharibifu huo.