Mwili wa msichana mwenye umri wa makamo ulipatikana umetupwa kando ya barabara kuu ya Nairobi kuelekea Nakuru mnamo siku ya Alhamisi.
Mwili huo ulipatikana umetupwa mtaroni katika eneo la Ihindu na watu waliouwa wakielekea kwenye timbo asubuhi, na ulichukuliwa na polisi kutoka kituo cha Magumu.
Inakisiwa huenda marahemu ambaye hakutambulika kwa jina, aliuawa mahala pengine na kisha mwili wake kutupwa eneo hilo.
Mkaazi wa eneo hilo Patrick Gitau alisema mwili huo ulikuwa na nguo zote lakini ulikuwa na ishara za kugongwa kwenye kichwa kwa kifaa butu pamoja na alama za kunyongwa kwenye shingo.
OCPD wa eneo hilo Yawa Chome alidhibitisha tukio hilo.
“Maafisa wetu waliuchukua mwili huo, na sasa umo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha. Uchunguzi umeanzishwa, lakini kama kuna yeyote amepoteza mtu wa familia ni vyema kuangalia kama ni yeye” akasema Chome.