Polisi mjini Mombasa wanachunguza kisa kimoja ambapo mwanamke anadaiwa kujifungua mtoto mchanga na kisha kumtupa katika jaa la taka katika eneo la Maweni, Kisauni, siku ya Jumanne.
Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni Richard Ngatia alisema kuwa walipokea habari hizo kutoka kwa umma na kuchukua hatua ya kuanza uchunguzi.
Aidha, kulingana na mkaazi mmoja, walimpata mtoto huyo akiwa tayari amefariki na kutoa ripoti kwa idara ya usalama eneo la Kisauni.
Polisi walifika mahala hapo kuondoa mwili ya mtoto huyo.