Mwili wa wanafunzi aliyeripotiwa kupotea wiki mbili zilizopita huko Likoni umepatikana katika ufuo wa bahari wa Shelly Beach.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na mzee wa mtaa wa eneo hilo Bwana Njagi mwili huo ulipatikana katika ufuo huo hapo jana jioni. 

Njagi anasema kuwa mwili huo unaweza kutambulika iwapo ni wa mwanamke au mwanamume japo ulikuwa umeoza kwa kiasi cha kutoweza kutambua sura kwa haraka.

Njagi anasema kuwa kulingana na hali ya mwili huo, mwanafunzi huyo ni dhahiri kuwa alibakwa kabla ya kutendewa kitendo hicho kiovu ndani ya bahari.

Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba babake mwanafunzi huyo alipiga ripoti kwa maafisa wa polisi kuwa mtoto wake alikuwa amepotea na kwamba mwanafunzi huyo alikuwa wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Puma eneo la Likoni na alikuwa mwenye umri wa miaka kumi na sita.

Kulingana na Ezekiel Ombaso babake mwanafunzi huyo mwanawe alipotea nyumbani tarehe nne mwezi jana na pindi tu alipobaini kuwa mwanawe amepotea alipiga ripoti kwa takribani vituo vyote vya polisi eneo hilo ili kupata msaada wa kusaidiwa kujua aliko mwanawe.

Aidha Simba amesema kuwa tayari uchunguzi wa kina utafanyika ili kubaini chanzo zha mkasa na wahusika wa mkasa huo.

Hata hivyo mwili wa mwanafunzi huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Pwani.