Mwili wa mwanamume mmoja wa umri wa makamo umepatikana kando ya barabara moja katika kijiji cha Getare lokesheni ya Mosocho kaunti ya Kisii ukiwa na majera kichwani na shingoni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo ambao walishuhudia kisa hicho walisema huenda mwanamume huyo aliuliwa sehemu tofauti na mwili wake kutupwa katika sehemu hiyo sababu si mkaazi wa maeneo hayo.

“Marehemu si mtu wa sehemu hii huenda aliuliwa sehemu tofauti na mwili wake ukatupwa katika sehemu hii ya Mosocho,” alihoji Daniel Maeba mkaazi wa eneo hilo.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kisii Level 5 huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Visa vya aina hiyo vimekuwa vikiendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbali za kaunti za Kisii na Nyamira katika siku za hivi karibuni na kiini chake bado kimesalia kuwa kitendawili.