Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi katika hafla ya awali. [Picha/ softkenya.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameibuka mshindi baada ya kura za mchujo za chama cha ODM kuregelewa katika baadhi ya vituo katika eneo bunge hilo.Mwinyi ameibuka mshindi kwa kura 4,974 huku mpinzani wake Goshi Ali akiwa na kura 1142.Mwinyi alitiwa mbaroni siku ya Jumamosi wiki mbili zilizopita baada ya kuzua fujo wakati wa kura hizo za mchujo.Kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Mombasa.Katika mchujo huo, wawakilishi wadi wote walioko madarakani walipoteza nafasi zao, isipokuwa mwakilishi wa Wadi ya Kipevu Ibrahim Kando.Atakaepeperusha bendera ya ODM katika Wadi ya Changamwe ni Bernard Ogutu, huku Junior Wambua akiteuliwa katika Wadi ya Chaani.Frederick Okolla aliibuka mshindi katika Wadi ya Port Riez kwa kura 430, na katika wadi ya Airport Ibrahim Bomoa alipata ushindi kwa kura 600.