Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha Ugavana Kaunti ya Mombasa katika uchaguzi wa 2022.
Mwinyi alisema kuwa wakaazi wa eneo bunge la Changamwe wanatambua juhudi zake za kuwaletea maendeleo na kumsukumu kuwatumikia wakaazi wa Mombasa kama gavana mwaka wa 2022.
Alisema kuwa ukosefu wa maendeleo na utekelezaji wa miradi mwafaka katika Kaunti ya Mombasa unatokana na kuzembea kazini kwa viongozi wa kaunti.
"Wakaazi wenyewe wa Changamwe wamependekeza niwanie kiti cha ugavana Mombasa mwaka wa 2022 ili niwaletee watu wa Mombasa maendeleo. Nitafanya vile wakaazi wa Changamwe wamependekeza,” alisema Mwinyi siku ya Jumatatu.
Wakati huo huo, alipongeza juhudi za Waziri wa Elimu nchini Dkt Fred Matiang'i kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inaboreshwa zaidi.
Mbunge huyo alisema kuwa uchomaji wa mabweni shuleni unatokana na hali ya walimu kutojali maslahi ya wanafunzi.
Msukumo wa Mwinyi kuwania Ugavana mwaka wa 2022 unatokana na kutofautia kisiasa na baadhi ya viongozi wa Mombasa pamoja na wakaazi wa Changamwe kukosa maendeleo mwafaka.