Jengo la Mahakama ya Mombasa. [PIcha/ the-star.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ya Mombasa imemfunga mwanamume mmoja kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la wizi wa redio.Juma Kanganyi anadaiwa kuiba redio hiyo yenye thamani ya shilingi 23,3000 katika eneo la Mwembe Tayar jijini Mombasa.Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa Kanyangi alitekeleza kosa hilo mnamo Disemba 28, mwaka jana.Mshtakiwa huyo alikubali madai hayo siku ya Jumatano mbele ya Hakimu Juliet Kasam.“Kweli niliiba radio hiyo na naomba msamaha. Sitorudia tena kosa hili,” alisema Juma.Akitoa uamuzi wake, Hakimu Kasam aliagiza Kanganyi kufungwa kifungo cha miezi sita jela ama alipe faini ya shilingi 20,000.