Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 72 katika kijiji cha Sengera, lokesheni ya Kitutu mashariki, kaunti ya Nyamira ameuawa na umati wa watu baada ya kudaiwa kuwa mchawi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumapili,  chifu wa lokesheni hiyo Tom Ndege alisema kuwa mzee huyo aliuawa na umati wa watu baada ya kudaiwa 'kumtembeza' mtoto wa nduguye nyakati za usiku na kuwakama ng’ombe wa majirani nyakati hizo hizo za usiku.

“Mzee huyu alidaiwa kuwa amekuwa akiwaroga wakazi wa kijiji hiki cha Sironga na kukama ng’ombe wa majirani, na kusumbua wakazi kupitia ushirikina na watu leo walimkimbiza na kumvahamia na kumuua,” alisemaNdege.

Chifu Ndege aidha alisema wakazi hao walichoma nyumba tatu za mzee huyo aliyeuawa papo hapo

Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha Keroka huku uchunguzi ukiendelea kufanywa kubaini ukweli halisi wa mambo.