Juhudi za kutatua mzozo kuhusu kufungwa kwa kampuni zinazomilikiwa na familia ya Gavana wa Mombasa Hassan Joho nje ya mahakama bado hazijazaa matunda.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yamebainika baada ya mawakili wa pande hizo mbili kuambia Mahakama kuu ya Mombasa kuwa bado hawajapata suluhu la kudumu.

Baada ya kusikiza mawakili wa pande zote mbili siku ya Jumatano, Jaji mkuu Enyara Emkukhule aliwaongezea wasimamizi wa pande zote mbili muda wa kumaliza mzozo huo.

Itakumbukwa kuwa usimamizi wa Halmashauri ya Bandari KPA na wamiliki wa kampuni za Autoport na Portside walielewana kumaliza mzozo huo nje ya mahakama.

Hii ni baada ya KPA kuzifunga kampuni hizo mwezi Februari mwaka huu.

Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 10, mwaka huu.