Huenda mzozo wa kimpaka kati ya serikali za kaunti ya Nyamira na ile ya Kisii ukachukua mkondo mpya baada ya serikali ya kaunti ya Kisii kutaka kujenga kwenye ardhi inayozozaniwa na kaunti hizo mbili. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na ujumbe wa barua, katibu wa uajiri katika kaunti ya Nyamira Erick Onchana alimwandikia katibu wa kaunti ya Kisii Johnstone Ndege ni kwamba serikali ya kaunti ya Kisii ilichukua hatua yakutaka kustawisha kituo cha mafunzo ya kilimo na kituo cha idara ya madaktari wa mifugo bila kuihuzisha serikali ya kaunti ya Nyamira.

"Inawezekana aje kwamba serikali ya kaunti ya Kisii inaweza chukua jukumu lakustawisha vituo hivyo viwili ikizingatiwa kwamba vituo hivyo vingali vina utata wa umiliki kati ya serikali ya kaunti hii na ile ya Kisii," alisema Onchana. 

Onchana, aidha, alisema kuwa maeneo hayo yanayozozaniwa yamo kwenye himaya ya kaunti ya Nyamira kwa mujibu wa mipaka ya kiutawala na siasa na anashangazwa na sababu ya inayoifanya serikali ya kaunti ya Kisii kutaka kustawisha maeneo hayo bila kuihuzisha kaunti ya Nyamira.

"Ikiwa maeneo hayo yanayozozaniwa yanastahili kustawishwa ingelikuwa bora iwapo serikali ya kaunti hii ingehuzishwa kwa maana kituo cha mafunzo ya kilimo na kile cha idara ya madaktari wa mifugo vimo katika himaya ya kaunti hii kulingana na mipaka ya kiutawala na siasa," aliongezea Onchana.