Mzozo baina ya mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu umeibuka tena.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya yanajiri baada ya Nelson Marwa kuyakashifu mashirika ya MUHURI na Haki Africa kwa kupinga mauaji ya wasichana watatu wanaodaiwa kutekeleza shambulizi la kigaidi katika kituo cha polisi cha Central.

Marwa amekosoa mashirika hayo kwa kile alichokitaja kama kuchochea wananchi kutekeleza uhasama baada ya mauaji hayo.

“Mashirika hayo yanasambaza propaganda katika mitandao ya kijamii kwa nia ya kuchochea wananchi na kusababisha uhasama baada ya tukio hilo,” alisema Marwa.

Shirika la MUHURI limepinga madai hayo, na kusisitiza kuwa jukumu lao kikatiba ni kutetea haki za binadamu wala sio kuendeleza uhasama kama inavyodaiwa na Marwa.

“Sharti sheria kufuatwa katika kukabiliana na wahalifu, sio kutekeleza mauaji kila wakati,” alisema Hassan Abdi Abdille, mkurugenzi mkuu wa Shirika la MUHURI.

Mashirika hayo mawili yanatambulika kwa kuikosoa idara ya ulinzi kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na wahalifu.