Ziara ya nabii mashuhuri David Owuor katika nchi ya Nigeria mwishoni mwa mwezi uliopita haikufaulu baada ya nabii huyo kushindwa kufanya miujiza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ziara ya Dkt Owuor katika taifa hilo la Afrika Magharibi ilitarajiwa kuwa hafla kubwa huku mabasi ya abiria yakibeba ujumbe kuhusu ziara hiyo na televisheni mmoja ya kibinafsi ikipewa mkataba wa kurekodi na kutangaza shughuli zake nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya ThisDayLive.com, wakaazi wa Nigeria waliokutana na Dkt Owuor katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Mohammed, walitaka kutendewa miujiza lakini nabii huyo akishindwa kutekeleza matakwa yao.

Inadaiwa kuwa nabii huyo alikataa 'kumbariki' mwanamume mmoja aliyekuwa amevaa rozari hadi pale alipotoa ishara hiyo ya 'kuudhi' ya kidini.

"Owuor hukumbwa na unyanyapaa wa mhubiri bandia hata nchini Kenya, huku viongozi wa kidini wanaoheshimika wakijitenga naye,” ilisema tovuti hiyo.

Aidha, tovuti hiyo iliripoti kuwa ingawa nabii huyo alisisitiza kwamba vipofu watapata kuona, hakuna kipofu wala kilema aliyepata uponyaji.

Owuor alijitahidi kudhibitisha kipawa chake cha uponyaji nchini Nigeria, lakini ilikuwa ni kama Mungu alikuwa amemsahau.

Tofauti na mikutano yake ya maombi nchini Kenya yanovutia umati mkubwa, mkutano wa Dkt Owuor nchini Nigeria uliofanyika katika eneo la kuegesha magari mjini Lagos, ulisemekana kuwavutia watu chini ya 500.