Halmashauri ya kitaifa ya kukabiliana na dawa za kulevya Nacada imemlaumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kutoa ufadhili kwa ustaawishaji wa miraa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika kikao na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, mkurugenzi mkuu wa kitaifa wa Nacada sheikh Juma Ngao, amesema hatua ya rais kutenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuimarisha ukulima wa miraa ni jambo la kisiasa.

Ngao amesema serikali imeenda kinyume na mapendekezo waliompa rais kuhusiana na zao hilo la miraa, licha ya kima kikubwa cha pesa za mlipaji kodi kutumika kufanikisha utafiti wa madhara ya miraa.

Kadhalika ngao amesema ukosefu wa nguvu za kisheria kushika na kushtaki wanaokiuka sheria za utumizi wa mihadarati imekua changamoto kufanikisha vita dhidi ya dawa hizo.

Siku ya Ijumaa rais Uhuru Kenyatta alitia sahihi mswada ambao sasa ni sheria kwmaba miraa ni miongoni mwa mazao ya biashara.

Zaidi rais ameunda jopo litakalotafiti changamoto zote zinazokumba biashara ya miraa ili ziweze kushughulikiwa na serikali.