Mamlaka ya kusimamia utumizi wa dawa ya kulevya nchini NACADA imeelezea wasi wasi wake dhidi ya idadi kubwa ya watu walioadhiriwa na dawa hizo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Aidha mamlaka hayo imehoji kuwa takriban wakenya milioni tatu wameadhiriwa na aina mbali mbali ya dawa za kulevya ikiwemo pombe haramu.

“Hali hii inafanywa kuwa mbaya zaidi na idadi kubwa ya wanafunzi wanaotumia dawa za kulevya wakiwa shuleni na ikiwa hatua ya mapema haitachukuliwa basi huenda tukawa na kizazi kilichooza,” mwenyekiti wa NACADA John Mututho alisema.

Akizungumza Jumatatu mjini Naivasha, Mututho alisema kuwa Kenya haina uwezo kamili wa kutibu hali hiyo ila tu kwa kubuni teknolojia itakayowasaidia walioadhirika.

Kulingana naye teknolojia hiyo imefanya kazi nchini India na hutumia mbinu ya kuwajenga waathiriwa fikira moyoni(Implant) kuwatibu na kuwarekebisha wale waliohadhiriwa na dawa hizo.