Nyota Ndogo, msanii kutoka Mombasa, amezua ati ati katika mitandao ya kijamii baada ya kuandika ujumbe kuhusiana na siasa za hapa nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Nyota aliandika kwa ukurasa wake wa Facebook kuwa anahisi ipo siku atakuwa rais wa Kenya, na ana imani Rais Uhuru Kenyatta atamuunga mkono.

"Sijui kwanini nahisi kua one day am gonna be the president of the country, alafu naona kama Rais Uhuru atanisapoti tu sana.”

Kauli hii inajiri huku joto la kisiasa likiendelea kupanda humu nchini, ikizingatiwa imebakia miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Kwingineko, siku chache tu baada ya Donald Trump kuteuliwa kuwa Rais wa Marekani, Susumila alitoa hisia zake kuhusu Wakenya na uchaguzi wa Marekani.

"Sasa sisi twashangaa wenzetu kumpigia kura Trump na sisi huku kila mwaka twaingiza viongozi wafisadi bungeni. Watu wanakufa kwa njaa na hawashughuliki, wananchi wanapitia dhulma za kila aina, wakija mwakani tunawapa tena kura. Mimi naona tungejishangaa sisi wenyewe kwanza," alisema Susumila.