Siku mbili tu baada ya washukiwa wa ujambazi kuivamia familia ya Geoffrey Ochoki na mkewe Jemima Nyamisa katika Kijiji cha Gekonge eneo bunge la Mugirango kaskazini, naibu chifu wa kata ya Bokeira Hezron Ongaro ameshtumu kisa hicho. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wanahabari kwenye eneo la tukio siku ya Jumatatu, Ongaro aliwataka wakazi wa eneo hilo kupiga ripoti kwenye kituo chochote cha polisi ikiwa kuna watu wanao washuku kutekeleza unyama huo.

"Ni ombi langu kwa wakazi wa eneo hili kupiga ripoti kwa kituo chochote cha polisi kuhusiana na washukiwa waliotekeleza unyama huu ili hatua kuchukuliwa," alisema Ongaro. 

Ongaro aidha aliitaka serikali ya kitaifa kujenga kituo cha polisi katika eneo la Nyamusi ili kuwahudumia wakazi wa maeneo hayo kwa saa 24, huku pia akiitaka serikali kuhakikisha gari la kufanya oparesheni linatumwa katika eneo hilo.

"Kwa sababu ya utovu wa nidhamu ambayo tunaendelea kuhushuhudia katika eneo hili kwa mda sasa yafaa serikali ya kitaifa ijenge kituo cha polisi hapa Nyamusi ili kiwahudumie wakazi saa 24," aliongezea Ong'aro.

Miili ya wenda zako inaendelea kuhifadhiwa kwenye kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kibinafsi ya HEMA kule Kisii, huku majeruhi wakiendelea kupigania maisha yao kwenye hospitali kuu ya Kisii.