Naibu Gavana wa kaunti ya kisii, Joash Maangi, amewaomba viongonzi wote wa kaunti ya kisii kujiunga pamoja kuwasaidia wananchi na kuwafanyia maendeleo .

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika kanisa la kiadventista la Getare iliyoko eneo bunge la Bomachoge Chache kwa hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa hilo Maangi alisema umoja kati ya viongonzi wote utaleta manufaa kwa wakaazi wa kaunti ya kisii.

Aidha, naibu huyo alisema viongonzi wa serikali ya kaunti ya kisii wanashirikiana na kuwaomba wabunge wa maeneo bunge mbalimbali katika kaunti ya kisii na seneta waungane pamoja na kuwatumikia wananchi kimaendeleo kikamilifu.

“Serikali ya kaunti ya Kisii iko imara. Nawaomba wabunge wote wa maeneo bunge katika kaunti hii ya Kisii tuungane pamoja tufanye kazi kwa wananchi kwa mapenzi ya Mungu,”alisema Maangi.

Wakati uo huo, Maangi alisema wananchi wa kaunti ya kisii watanufaika kimaendeleo ikiwa viongozi wote watashirikiana pamoja na kuyatimiza yale waliyowahidi wananchi haswa wakati wa kampeini.

“Ushirikiano kwa viongozi wote wa kaunti na wale wa serikali ya kitaifa kutainua  maendeleo katika eneo la kisii,” aliongezea Maangi.

Kwa upande mwingine wananchi waliokuwa kwa hafla hiyo walifurahishwa na ombi hilo la Naibu Gavana Maangi na kusema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu na kuomba viongozi kukubali ombi la naibu huyo na kufanya maendeleo katika eneo la kisii.

“Viongozi wote wakishirikiana pamoja sisi wananchi tutafanyiwa yale yote walituahidi maana hakutakuwa na yeyote wa kuyakana maendeleo hayo,” alihoji George Orero mkaazi wa kaunti ya Kisii.

“Tunaomba viongozi wetu kukubali ombi hilo la naibu gavana na tuko tayari kufurahishwa kimaendeleo,”aliongezea Orero.