Naibu Kamishna wa Mombasa ameupongeza mpango wa Nyumba Kumi kwa kuimarisha usalama katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu katika ufunguzi wa kongamano la uhamasisho lililoandaliwa na kamati ya kitaifa ya mpango huo wa Nyumba Kumi, Bwana Mahmoud Salim alisema kuwa viwango vya usalama vimeimarika katika kaunti hiyo.

"Nina imani na mpango huu unaonekana kufaulu katika kuboresha usalama kwa kuwa usalama ni jukumu la kila mwamanchi wala sio kazi ya maafisa wa polisi pekee,” alisema Salim.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kitaifa wa mpango huo wa Nyumba Kumi Bwana Joseph Kaguthi alitoa wito kwa kila mtu kushirikiana kwa dhati kwenye harakati za kukabiliana na uhalifu katika maeneo yao ya makaazi.

"Itakuwa jambo la busara kuwashirikisha wanawake kwa wingi katika mpango huu,” alisema Bwana Kaguthi.