Naibu kamishna wa Kaunti ya Kisii Phillip Soi amewahakikishia wakaazi wa wadi ya Magenche Kaunti ya Kisii kuwa usalama utawekwa dhidi yao kikamilifu.
Haya yanajiri baada ya wakaazi hao kuenda hadi ofisi yake iliyoko mjini Kisii siku ya Alhamisi kulalama kuwa wamehofiya usalama wao baada ya baadhi ya viongonzi wa eneo hilo ambao ni machifu na manaibu wao kutengeneza kikundi cha vijana kuwatisha wakaazi hao dhidi ya uongonzi wa eneo hilo.
“Kuna kiongonzi wetu ambao ameunda kikundi cha vijana na kugawa na kututishia maisha ndio maana tulikuja hapa kwa kamishna kutafuta msaada,” alihoji Ken Marando mkaazi aliyeongoza wakaazi wengine.
“Sisi hatutaki ugomvi tunataka amani penye tunaishi haya mambo yanaletwa na baadhi ya machifu sisi hatutaki kamwe na tunayakana,” aliongeza Marando.
Wakati huo huo, naibu kamishna wa Kisii Phillip Soi alisema hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yao ili kuhakikishiwa usalama wao na kuzuia ugomvi huo katika mipaka yao hasa katika mpaka wa Wakisii na Wamaasai.
Katika mpaka huo kumeshuhudiwa wizi wa mifugo kwa muda mrefu sasa lakini suluhu itapatikana hivi karibuni hayo ni kwa mujibu wa naibu kamishna.