Naibu Kamishna wa Likoni Bwana Geoffrey Omoding amepata uhamisho hadi Kaunti ya Machakos katika wadhifa huo huo.
Nafasi yake Likoni imechukuliwa na Naibu Kamishna wa Kaunti ya Machakos Bwana Francis Kimathi.
Omoding alihudumu Likoni kwa muda wa miezi minne pekee.
Naibu wa mkuu wa polisi katika Kituo cha Likoni Fredrick Juma pia amepata uhamisho mpaka Nakuru kwa wadhifa kama huo.
Haya yanajiri wiki tatu baada ya aliyekuwa Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki kupata uhamisho hadi Kaunti ya Samburu.
Omoding atakumbukwa kwa utendakazi wake baada ya vijana 28, wanaoaminika kuwa wanachama wa magenge yanayowahangaisha wakaazi, kujisalimisha kwa polisi.