Wakaazi wa kaunti ya Nakuru sasa hawatafurajhia ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege, baada ya mamlaka ya kusimamia viwanja vya ndege nchini KAA kusema kwamba imekosa nafasi inayostahili ya mradi huo.
Tangazo hilo limejiri miezi mine baada ya serikali ya kaunti ya Nakuru kuwekeana mkataba wa ujenzi wa uwanja huo na KAA, manmo Novemba 2015.
Badala yake serikali ya kaunti ya Nakuru sasa imesema itaanzisha mpango wa kukarabati viwanja vyote vidogo vya ndege vilivyoko katika kaunti hiyo.
Gavana Kinuthia Mbugua amesema “hatua hiyo ni pigo kubwa kwa kaunti yetu kwani imeadhiri ahadi tuliyoweka wakati tukifanya kampeini ya mwaka 2013”.
“Kama uwanja huo ungetengenezwa ungefungua maswala ya uwekezaji na biashara hususan kwa wakulima wa maua ambao wangeweza kusafirisha bidhaa zao bila ya kuelekea Nairobi” akasema Mbugua baada ya hafla ya gavana mtaani mjini Naivasha kwa siku ya pili.