Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae ametangaza kuwa waliopoteza jamaa zao katika shambulizi lililotekelezwa katika chuo kikuu cha Garissa kuenda moja kwa moja hadi ofisi za maafisa wake wa kaunti wakiwa na vitambulisho ili kutia sahihi na kupokezwa pesa za ufadhili wakati wowote.
Akiongea wakati wa sherehe ya maombi ya upamoja yaliyofanywa kwa waliofiwa, Ongwae alisema waliopoteza wenzao, ambao ni familia kumi na mbili, katika kaunti hiyo watakabidhiwa shillingi 100,000 huku Ongwae akiahidi kuajiri mtu mmoja kutoka familia hizo katika serikali ya kaunti.
Walionusurika kifo nao watapokezwa shilling 10,000, huku Ongwae akiuliza serikali kuu kuwachukulia hatua waliotekeleza mashambulizi hayo na kutoweka,na kusema hawatakubali kushambuliwa kila mara,
“Hatutakubali sisi wakisii kushambuliwa kila wakati, heri usalama wa kutosha kuimarishwa nchini, nimesema hatutakubali na hatutakubali kamwej,” alisema Ongwae.
Wakati huo huo, Gavana alikashfu kitendo hicho cha mauaji ya kila mara, na kusema sharti serikali ya kitaifa iwajibike kwa usalama, huku zaidi ya watu takriban 10,000 wakiunga mkono ombi la gavana kwa serikali kuu.
Aidha, waliofiwa waliomboleza kwa machonzi, huku miili ya waliofariki ikisafirishwa nyumbani kwa mazishi.
Wanachi nao waliomba serikali kuwahakikishia usalama wao kikamilifu.
Waliohudhuria sherehe hiyo ya maombi ni seneta wa Kisii Chris Obure, mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kisii Mary Otara, wawakilishi wa wadi mbalimbali, na wabunge.