Katibu mkuu wa chama cha Ford Kenya Kaunti ya Mombasa Yasser Bajaber amesema kuwa mrengo wa kisiasa wa NASA umejipanga vyema kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Bajaber alikanusha madai kuwa kuna baadhi ya viongozi watapewa tiketi za moja kwa moja katika mrengo huo.

Bajaber alisema kuwa hizo ni porojo tu kwani kila kiongozi atashiriki kura za mchujo.

Bajaber aidha alisema kuwa kila chama katika mrengo huo kitahusishwa kikamilifu bila unyanyasaji katika maswala ya uongozi, kwa kuwa lengo lao kuu ni kuona wananyakua nyadhifa mbalimbali za uongozi ifikapo uchaguzi mkuu.

Aidha, ameahidi kushirikiana vyema na kiongozi yeyote atakeyepewa mamlaka ya kupeperusha bendera ya uraisi ifikapo wakati wa uchaguzi mkuu.

Wakati huo huo amewataka wananchi kuwa wangalifu na hata kujitenga na viongozi wabinafsi.