Viongozi wa mrengo wa NASA Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wakiwahutubia wakaazi wa Meru hapo awali. [Picha/ radiotaifa.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi katika mrengo wa NASA wamewaonya wakaazi wa Pwani kuwa waangalifu na kutahadhari dhidi ya njama za chama cha Jubilee kikiongozwa na naibu wa rais William Ruto.Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wasema kwamba azma ya Ruto ya kusafiri kwenda Pwani kila kuchao ni ya kushangaza na kutiliwa shaka.Viongozi hao walionya kuwa huenda Ruto anapanga njama ya kunyakua mashamba katika eneo hilo.Walidai kuwa kuna kiongozi wa ari ya juu katika Jubilee anayesemekana kuwa amenunua mashamba makubwa huko Kwale.Waliwarai waakazi wa Kwale kutahadhari dhidi ya watu wanaomezea mate madini yaliyoko Pwani.Wakiongea huko Kinango, viongozi hao walisema kuwa ni dhahiri kwamba Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Ruto wamegadhabishwa na umoja ulioko kwenye mrengo wa upinzani.“Yeyote kati yetu wanne anaweza akawa rais katika uchaguzi ujao. Lazima tukomboe Kenya kutokana na uongozi mbaya wa Uhuru,” alisema Wetangula.Vilevile viongozi hao walisema kuwa yapaswa Ruto afanyiwe uchunguzi ili ibainike mali yake ilikotoka.Aidha, walimkea Gavana wa Kwale Salim Mvurya kwa madai kuwa anajipendekeza kwa serikali ili ajinufaishe kibinafsi.