Mamia ya wakaazi wa wadi ya Majengo eneo bunge la Mvita wamejitokeza kwenye kambi ya matibabu ya bure yaliyozinduliwa rasmi na wakfu wa Sheriff Nassir na serikali ya kaunti ya Mombasa katika eneo bunge hilo kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa hepatitis A.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na afisa mkuu wa afya gatuzi dogo la Mvita Anwar Ali, tangu mwezi Januari takribani watu 88 wameathirika na homa hiyo ambayo inazidi kuenea katika kaunti nzima.

Anwar amesema homa hiyo husababishwa sana na maji yaliyotangamana na virusi vinavyosababisha homa hiyo.

Rashid Sumba ni mmoja wa walioathirika na hepatitis A ambaye ameweza kuhudumiwa baada ya kukosa huduma katika hospitali kuu ya mkoa hapo jana na anasimulia dalili za ugonjwa huo.

Wakati uo huo wakaazi wa eneo bunge la Mvita wametoa shukrani zao kwa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.

Abdulswamad amesema ameandaa matibabu hayo ili kuhakikisha wakaazi wake wako na afya bora pamoja na kuwakinga na maradhi yanayochipuka.