Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amewakashifu viongozi waliouhama mrengo wa upinzani na kujiunga na chama cha Jubilee.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Nassir amedai kuwa ulafi na ubinafsi wa viongozi hao ndio uliowasababisha kuchukua hatua hiyo.

Akizungumza Mjini Mombasa, Nassir alisema kwamba viongozi hao walioasi Chama cha ODM kamwe hawana nia yoyote ya kubadili hali ya maisha ya wakaazi wa Pwani.

“Viongozi waliohamia Jubilee wamesukumwa na maslahi yao ya kibinafsi na wanalenga kujinufaisha wao wenyewe na wala sio wakaazi wa Pwani,” alisema Nassir.

Nassir aliikosoa serikali ya Jubilee kwa kusema kwamba haijatekeleza maendeleo yoyote katika eneo la Pwani.

Aliwatahadharisha wakaazi dhidi ya kuwapigia debe viongozi wa Jubilee, kwa madai kuwa serikali haiwajali Wapwani.