Makamishina wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC wameshauriwa kuitikia wito wa kuondoka afisini ili makamishina wapya wachukuwe fursa ya kusimamia uchaguzi ujao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ushauri huo umetolewa baada ya makamishina hao kusimama kidete katika azma yao yakusalia afisini huku wakiombwa kujiuzulua jinsi wameombwa na mashirika mbalimbali.

Akizungumza nasi mwanasiasa katika eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira Victor Ogeto alisema itakuwa vyema kwa makamishina hao kujiondoa afisini baada ya imani kukosekana haswa kutoka kwa wakenya wa tabaka mbalimbali.

Ogeto aliwashauri makamishina hao kuitikia wito wa muungano wa Cord, makanisa na wakenya wengine.

"Makamishina wa IEBC wamekuwa wakiombwa kujiondoa maana wengi wamepoteza imani nao mimi nawashauri waitikie wito wa kujiondoa ili Kenya kuwa na amani kwani hatuna imani na tume hiyo," alisema Ogeto.

Siku ya Jumatatu wakenya haswa wafuasi wa mrengo wa Cord katika kaunti ya Nyamira waliandamana kuelekea katika afisi za IEBC ili kuwaondoa huku maandamano sawia na hayo yakifanyika Nairobi, Kisumu na sehemu zingine nchini.