Viwango vya uchochezi katika mitandao nchini hasaa ya kijamii vinazua wasiwasi hasaa wakati huu taifa linapojiandaa tayari ka uchaguzi mkuu mwaka 2017.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamishna katika tume ya uwiano na maridhiano nchini NCIC Linda Ochielo amesuta hatua ya wananchi kutumia mitandao ya kijamii kuelezea hisia zao kupitia jumbe zinazoeneza chuki kwa matusi.

Ochiele anasema hali ya uchochezi na chuki unatatiza umoja wa taifa.

''Kama tume tumeweka mipango mahsusi itakayoona kuwa matukio yote ya kimtandao hasaa ya kijamii yanafuatiziwa kikamilifu na hivyo ipo haja kwa wakenya kuepukana na matamshi ambayo ni ya uchochezi kwa maana sheria haitamsaza yeyote mwenye kueneza chuki nchini,'' Ochielo alisema.

Ameongeza kuwa tume ya NCIC inaweka juhudi kuhakikisha kuwa panabuniwa mfumo wa kufuatilia matukio kwenye mitandao ya kijamii hali ambayo inalenga kusaidia katika hatua za kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.