Tangu siku za utotoni Samuel Nyabote alikuwa na matumaini ya kusoma kupata ajira na kusaidia jamaa zake.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwa sasa matumaini yake hayatatimia baada ya magaidi wa Al Shabaab kukatiza ndoto zake.

Nyabote, yatima, ni mmoja wa wanafunzi 148 ambao waliuawa na magaidi katika chuo kikuu cha Garissa University.

Nyabote alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.

Kwa mahojiano na mwandishi huyu, binamuye Nyabote, John Ombogo anasema kuwa familia yao ilikuwa na matumaini na Nyabote kwani alikuwa bora masomoni.

“Tumelelewa pamoja. Tangu wazazi wake walikufa alichukuliwa na mama yangu na tumekuwa kama ndugu. Yeye alikuwa bora kwa masomo na tulikuwa na matumaini naye,” asema Ombogo. 

Nyabote ni mmoja wa wanafunzi ambao miili yao ilitambuliwa kupitia kwa sayansi ya vidole.

Ombogo alisema kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo (Alhamisi) na kuzikwa ijumaa (kesho) katika kaunti ya Kisii.

“Naskia uchungu kumpoteza binamu yangu. Kwangu ni kama ndugu,” asema Ombogo.  

Ombogo anaendele kusema kuwa pesa amabzo serikali inawapa waathiriwa haiwezi ikalinganishwa na maisha ya binadamu.

Serikali kuu imeseama kuwa itawapa fidia waathiriwa wa mkasa wa Garissa Sh100,000.