Mtalii mmoja alipata kukumbana na mauti hapo siku ya Jumapili mwendo wa saa tano asubuhi katika Mbuga ya wanyama ya Tsavo pale alipokanyagwa kanyagwa na ndovu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Fernando Mocclola, mwenye asili ya Kiitaliano, na mkewe walikuwa wamesajiliwa katika 'Swara camp' ambako kisa hiki kilitokea.

Inasemekana kwamba mtalii huyo mwenye umri wa miaka 66 alimwacha mkewe katika chumba akaenda kupiga wanyama hao picha katika sehemu yao ya kunywa maji ya mto Sabaki wakati kisa hicho kilipofanyika.

Mkuu wa polisi wa malindi anakisia kuwa huenda ndovu hao walikerwa na vile Mocclola alivyokuwa akiwasogea.

"Huenda aliwasogea karibu sana ndovu hao hadi wakakerwa na mmoja wao kumfukuza walipohisi wako katika hatari ya kushambuliwa," alisema mkuu huyo.