Ndugu wawili wanaokabiliwa na shtaka la kumshambulia na kumtishia mwanamke mmoja walifikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu shtaka hilo.
Wawili hao, Darlingtone Wahome na Priscilla Wahome wanadaiwa kumshambulia Priscilla Thiga, na kumtishia kwamba watamkatakata kwa panga tarehe Oktoba 26, 2015, katika kijiji cha Mbaru eneo bunge la Gilgil, Kaunti ya Nakuru.
Hata hivyo, wawili hao walikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu Doreen Mulekyo, na kuaachiliwa kwa baili ya Sh5,000 pesa taslimu.
Washtakiwa hao wanatarajiwa kurejea mahakamani Novemba 5, 2015.