Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkurugenzi wa halmashauri ya kitaifa ya kampeni dhidi ya madawa ya kulevya na vileo Nacada Sheikh Juma Ngao ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuunda jopo la ardhi za wakfu ili kusitisha ufisadi unaodaiwa kukita mizizi katika tume ya Waki.

Akizungumza na wakaazi wa kaunti ya Mombasa katika maadhimisho ya shereza za Jamhuri, Ngao alisema kuwa kuundwa kwa jopo hilo lingesaidia kuregesha zaidi ya bilioni 10 pesa taslimu za malipo za ardhi za Wakfu  na kuboresha maisha ya walimu wa dini wanaohubiri kuchochea ugaidi miongoni mwa vijana kwani ardhi zitaweza kutozwa ada kulingana na malipo wakati huu na kuongeza pato nchini.

Vile vile, Ngao aliitaka serikali kuifanyia mageuzi vipengele katika sheria ya tume ya Waki ili kuhakikisha wanaoteuliwa kuhudumia katika tume hiyo hawabagui makabila mbali mbali.

Kulingana na Juma, wahubiri wanaoeneza ugaidi miongoni mwa vijana hawana budi kupokea malipo kutoka kwa mabwenyenye wanaoendeleza ugaidi baada ya kupokea malipo duni.

Aidha, Ngao aliileza kuwa ardhi za wakfu zilitengwa na malipo yake kulipa walimu wa dini wa Madrasa, mashehe, wajane na mayatima ili kuboresha maisha na kuinua uchumi nchini.

Ngao alisema kuwa maeneo yaliyo na ardhi za wakfu ni Tudor, mkahawa maarufu wa Casblanca, hoteli ya Glory, miongoni mwa ardhi zingine nchini.

Vile vile Kamishna kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amewataka vijana kutotumiwa na mabwenyenye na kutatiza amani katika kaunti ya Mombasa, huku akiwataka kujitoa katika visa vya utovu wa nidhamu mbali kushiriki katika miradi ya ugatuzi nchini.

Hata hivyo, wagonjwa katika hospitali ya rufaa  katika kaunti ya Mombasa wameridhika  kupata afueni ya kutolipa malipo ya matibabu baada ya Hassan Joho kuamuru wagonjwa waliokosa malipo kuachiliwa huru ili kufurahia uhuru nchini na familia zao katika sherehe za maadhimisho ya Jamhuri.

Muuguzi wa hospitali ya rufaa Gladys Wambugo alifurahishwa na tangazo hilo na kuliita la kipekee tangu aanze kazi ya uuguzi nchini, huku akisema kuwa wagonjwa waliridhika na tangazo hilo baada ya kukaa katika hospitali licha ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Viongozi waliohutubia wakaazi wa Mombasa katika madhimisho ya sherehe za Jamhuri nchini wamewataka Wakenya kumaliza ufisadi katika idara mbali mbali zikiwemo za maafisa wa usalama, ukosefu wa usalama, vita dhidi ya madawa ya kulevya na vileo miongoni mwa matatizo mengine.