Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wakazi waliwazuia ng’ombe watano  ambao waliibwa kutoka kijiji cha Mongori wilayani Borabu, kaunti ya Nyamira.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ng’ombe hao walikuwa wa mjane mmoja katika wilaya ya Borabu huku habari ikisambaa dhidi ya wizi huo.

Kulingana na mkuu wa polisi wilayani Sotik Johnthan Ngala aliyezungumza siku ya Jumanne, ng’ombe hao walifumaniwa wakisafirishwa katika eneo la Kabkures sotik huku maafisa wa polisi wakifanikiwa kuwazuia.

Ngala aliomba wakazi kuendelea kushirikiana na polisi kupunguza wizi wa ng’ombe ambao umekithiri katika maeneo hayo.

“Tuliwazuia ng’ombe watano ambao walikuwa tayari wameibwa, tulipokezwa habari na tumerudisha ng’ombe hao kwa mwenyewe ambaye ni mjane wilayani Borabu,” alisema Ngala.

Aidha, wakazi wa eneo hilo walilalamikia hali hiyo ya wizi na kuomba maafisa wa polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa kutosha ili wasiendelee kukabiliwa na hasara ambayo imekuwa ikiendelea.