Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amesema kuwa afisi yake itahakikisha kuwa eneo bunge hilo linapata maji safi kwa matumizi ya nyumbani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea Jumamosi, Ngunjiri alisema wakaazi wa eneo hilo wamekuwa wakiteseka kutokana na ukosefu wa maji.

“Hapa watu wamekuwa wakiteseka sana kutokana na ukosefu wa maji, lakini sasa afisi yangu imejitahidi kuhakikisha wakaazi wote wanapata maji,” Ngunjiri alisema.

Ngunjiri alikuwa akizungumza katika eneo la Karuchwa Dundori wakati alitoa hundi ya shilingi milioni moja kwa wakaazi ili kufanikisha ununuzi wa pampu ya maji.

Wakaazi wa eneo hilo wamekuwa wakitembea zaidi ya kilomita tano kuteka maji.

“Eneo hili limekuwa likisahauliwa na viongozi waliopita lakini afisi yangu itahakikisha imeshirikiana na nyinyi,” Ngunjiri alisema.

Eneo la Karuchwa liko katika mpaka wa kaunti ya Nyandarua na Nakuru.

Mbunge huyo pia ameahidi kuwa watahakikisha kuwa kuna mashimo ya maji ya kutosha.