Mbunge wa Bahati Onesmus Kimani Ngunjiri ameapa kuimarisha miundo msingi ya elimu katika eneo bunge lake.
Ngunjiri ameyasema hayo wakati alipoongoza hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi ya Central, Engoshura.
Kwa mujibu wake, ujenzi wa madarasa hayo mawili utagharimu takriban shilingi milioni 1.4.
Shughuli hiyo itafadhiliwa na hazina ya maendeleo CDF eneo bunge la Bahati.
"Tunajua elimu ni nguzo muhimu kwa maendeleo, ndiposa nimeamua sharti tuimarishe miundo msingi kama vile darasa," alisema Ngunjiri.
Wakati uo huo, amewataka wazazi kushirikiana na walimu kufanikisha matokeo mema.